Jamvi

Tenzi Swahili

Posted on

Na Msarifu Glen Isaack

1.
leo nangiya humu,kidogo nikazuumu,
niueleze utamu,wa lugha ninofahamu,
lugha hii ni nujumu,tutumie nchini humu,
lugha yetu kiswahili,sote tuifurahie.

2.
msipapiye kwa hamu,lugha geni kufahamu,
za kwenu huwa muhimu,
hata kama mehitimu,
wazungu wamejaa humu,swahili wakifahamu,
lugha yetu kiswahili,mila katu hatuachi.

3.
tena tusitie sumu,kuuharibu utamu,
kufaulu ni vigumu,kiswahili kitadumu,
msoona umuhimu,mtaishia kuzimu,
lugha yetu kiswahili,afurika mashariki.

4.
wasemao ni kigumu,si matusi ashakumu,
nitawaita wazimu,waja wasio na hamu,
wasoona umuhimu,wa hii lugha ma’lumu,
lugha yetu kiswahili,fahari tuionee.

5.
nawasihi wanadamu,kiswahili kuhishimu,
sio tu kwa kielimu,bali kwa kila sehemu,
muwache kukilaumu,mkisema ni kigumu,
lugha yetu kiswahili,tutumie kotekote..

Kongamano la Kimataifa la Kiswahili Kufanyika Kigali, Rwanda

Posted on Updated on

Mwasisi wa taaluma ya Kiswahili, Shabaan bin Robert, na mojawapo ya vitabu vyake
Mwasisi wa taaluma ya Kiswahili, Shabaan bin Robert, na mojawapo ya vitabu vyake

 

Na Masrifu Glen Isaack

Kongamano kubwa la kimataifa kuhusu Kiswahili limepangwa kufanyika mjini Kigali, Rwanda Agosti mwaka huu. Kongamano hilo linalotarajiwa kuhudhuriwa na idadi kubwa ya washiriki wakiwemo walimu, wataalamu, watafiti, wanahabari, wasanii, maashiki na wakereketwa wa Kiswahili kijumla litang’a nanga mnamo tarehe 29 hadi 31 Agaosti. Kauli mbiu ya kongamano la mwaka huu ni “Kisahili ni tunu na johari ya Afrika” Miongoni mwa mada zitakazoangaziwa ni pamoja na ubunulizi katika Kiswahili na athari yake chanya kwa jamii. Nyingine ni pamoja na:

1. Ukweli kuhusus chimbuko la Kiswahili

2.mchango na athari za jumuiya ya Afrika mashariki kukifanya kiswahili kiwe lugha moja kwa afrika nzima.

3.kiswahili kama chombo cha ukombozi wa afrika.

4.kuwasilisha utamaduni wa mswahili kwa njia ya igizo.

5.”urari wa vina na mizani ndicho kitovu na uti wa mgongo wa ushairi wa kiswahili”kubali au kanusha dai hili kwa mifano yenye mashiko.

6.lugha ya kiswahili haikidhi matakwa ya sayansi na teknolojia inayokua kwa kasi kubwa barani afrika..jadili dai hili kwa mifano kuntu.

TANBIHI.
1. Wahadhiri na washiriki wengineo wanaweza kuandaa mada zao tofauti na hizi ili kuleta vionjo zaidi.

2 pia, mada hizi zinaweza kuwasilishwa kwa njia ya maigizo,ushairi,tenzi vitushi nk.

 

Maafisa Mafisadi

Posted on

Ninaingiya jukwani,Maafisa sikieni,
Nataja yalo moyoni,papa hapa ulingoni,
vitendo vyenu ni duni,kuliko vyote nchini,
Maafisa wa trafiki,mafisadi namba wani.

Mkiwa barabarani,vya haki hamthamini,
Munachukuwa mapeni,makosa hamuyaoni,
Mukipewa hamsini,hamuulizi kwa nini?
Maafisa wa trafiki,mafisadi namba wani.

Hamna akili vichwani,ni ukweli si utani,
Katu mi siwaamini,mwatutiya taabani,
Ni heri muwe nyumbani.nyinyi watu maluuni,
Maafisa wa trafiki,mafisadi mamba wani.

MSARIFU GLEN ISAACK
[12/06/13.]

Wanakwetu Zindukeni

Posted on

Na Msarifu Glen Isaack

Ninajitoma getini,
Machache kuwambieni,
Kwa makini sikizeni,
Muyatiye akilini,
Ufahamu duniani,
Huwa si kwetu Nyumbani,
wanakwetu zindukeni
Ukimwi watumaliza. . .

Tunazama maovuni,
Wengi wetu tunazini,
Tunapuuza uneni,
Wa kondomu mpangoni,
‘Twajijaza’ vitandani,
Eti ‘tunajiamini’,
Wanakwetu zindukeni,
Ukimwi watumaliza.

Uaminifu ndoani,
Ni bora sana jamani,
Wale wa kando Pembeni,
Katu usiwaamini,
Takutiya hatarini,
Ujipate kaburini.
Wanakwetu zindukeni,
Ukimwi watumaliza.

Nanyi vijana wandani,
Mapenzi si yenu fani,
Jali yanu ya usoni,
Ya muhimu maishani,
Musitafute mapeni,
Kwa nndiya ya kuzini,
Wanakwetu zindukeni,
Ukimwi watumaliza.

(2013) msarifu glen isaack